SIMULIZI: THE JOKER - Muuaji wa Siri Sehemu ya kwanza hii Hapa
- THE JOKER (Muuaji wa Siri) Sehemu ya Kwanza hii hapa: Katika Nchi ya Tanzania, jijini Mwanza, yapata saa tano za usiku, katikati mwa jiji la Mwanza eneo la Capri point, mtaa wa sita kutoka barabara Kuu ya kuingia katika jengo la Benki Kuu ya Tanzania, nyumba namba 43 nyumba ambayo geti lake lilikua la chuma kilichochakaa, Upande wa ndani kulikua na nyasi nyingi zilizoonyesha hazijapata kufyekwa takribani miaka miwili, pembeni mwa jengo lile kulikua na gari bovu aina ya land Cruiser rangi ya bluu, Lango la kuingilia ndani pembezoni kabisa mwa ukuta palikua na Pipa, ambalo ndani yake kulikua na karatasi zinaendelea kuwaka, humo ndimo alimojificha Joka Mtu, au kwa jina lingine unaweza kumuita The Joker, akiwa kasimama katika kioo kilichopasuka, shingoni akiwa kajifunga mnyororo mrefu uliofika hadi kwenye kiuno kisha kurudi tena shingoni na kushuka hadi chini, hakika ulionekana mnyororo mzito kwelikw...