SIMULIZI: THE JOKER - Muuaji wa Siri Sehemu ya kwanza hii Hapa

 - THE JOKER (Muuaji wa Siri)  Sehemu ya Kwanza hii hapa:


Katika Nchi ya Tanzania,  jijini Mwanza,  yapata saa tano za usiku, katikati mwa jiji la Mwanza eneo la Capri point,  mtaa wa sita kutoka barabara Kuu ya kuingia katika jengo la Benki Kuu ya Tanzania,  nyumba namba 43 nyumba ambayo geti lake lilikua la chuma kilichochakaa, 


Upande wa ndani kulikua na nyasi nyingi zilizoonyesha hazijapata kufyekwa takribani miaka miwili, pembeni mwa jengo lile kulikua na gari bovu aina ya land Cruiser rangi ya bluu, 

 Lango la kuingilia ndani pembezoni kabisa mwa ukuta palikua na Pipa, ambalo ndani yake kulikua na karatasi zinaendelea kuwaka,  humo  ndimo alimojificha Joka Mtu,  au kwa jina lingine unaweza kumuita The Joker,  akiwa kasimama katika kioo kilichopasuka,  shingoni akiwa kajifunga mnyororo mrefu uliofika hadi kwenye kiuno kisha kurudi tena shingoni na kushuka hadi chini,  hakika ulionekana mnyororo mzito kwelikweli ila kwa upande wake ilikua tofauti,  alijiangalia kwenye kioo huku akiendelea kutoa tabasamu,  Nywele zake zikiwa zimevurugika,  mfano wa Mwendawazimu,  mkono wake wa kulia ukanyanyuka na Moja kwa Moja ukaelekea upande wa kulia nakuchukua kikopo ambacho kilionekana kuwa na unga ndani yake akakifungua,  kisha akatoa sponji laini ndani yake,  nakuanza kujipaka vitu vyeupe usoni mwake mithili ya poda, alijipaka kwa kujizungushia unga ule mweupe kwenye mashavu yake, 

kisha akahamia kwenye paji lake la uso alipomaliza kujipaka alijiangalia tena kwenye kioo kisha akatoa tabasamu na kucheka kwa Sauti sana,  Sauti ambayo ilisababisha Mbwa aliyekuwemo ndani ya chumba kile kubweka kwa Sauti ya Uoga,  The Joker au Nyoka mtu alikua akipenda kukaa na Mbwa wake mweusi aitwae Podi,  


Podi alikua Mbwa Mzee asiye na meno ila Mkali kupindukia,  Joker alimgeukia Podi kisha akainama na kuongea nae kana kwamba anamuelewa "Nimependeza!?" Podi alibaki kumwangalia tu kisha Joker akanyanyuka na kujiangalia tena kwenye kioo kisha akajisemea "hakika mfupa wa binadamu wa kike Una rangi nzuri sana," akachukua baadhi ya unga aliojipaka kwenye shavu lake la kushoto kwa kutumia kidole chake cha kulia, akapeleka mdomoni na kujilamba,  kisha akacheka tena,  wakati akiendelea kujiangalia Gafla!!, Mlio wa simu uliita ukitokea kitandani, kitanda kilichoonekana hakijatandikwa vizuri ya pata mwezi, 


 Joker alikua hapendi sana tabia ya kupigiwa Simu, japo Simu ndio iliyokuwa ikimuunganisha na dunia ya nje,  yeye binafsi alikua akiamini ya kuwa yupo dunia ya kuzimu ila binadamu walimuitaji kwa ajili ya kupeleka roho za watu kuzimu,  sehemu ambayo anaamini yeye alikuwepo, alichukua Simu na kuitizama kwenye Kioo,  ilikua ni namba ya Lilian kwa Jina lililokua limeonekana kwenye kioo,  akachukua na kupokea Bila kuongea " Joker muda unaisha nenda chumba namba 9" Simu ikawa imekatwa. 


Kwa spidi ya ajabu Joker alijivua ule mnyororo aliokua amejifunga shingoni,  haikujulikana kwanini anapenda kuvaa mnyororo mzito vile shingoni, akaenda Moja kwa Moja hadi kwenye kabati kubwa lilokuwemo chumbani mule, nakulifungua,  walitoka panya wakikimbia kuelekea chini ya uvungu wa kitanda,  ndani ya kabati kulionekana kukiwa na mafuvu ya watu takribani tisa,  na silaha mbalimbali,  Joker aliendelea kupekua ndani ya kabati na kuvuta droo moja,  akatulia kwa muda kisha akaifungua,  ndani ya droo kulikua na silaha kubwa aina ya   AK47 ikiwa imefungwa kitambaa cheusi akaitoa silaha na kuipangusa vumbi,  akaendelea kuangalia kitu kingine cha kuchukua akaona boksi dogo la risasi,  akalichukua na kuliweka ndani ya koti kubwa jeusi alilokua amelivaa,  akarudi tena kwenye kioo na kuchukua rangi mfano wa damu na kujipaka mdomoni,  kisha akatabasamu na kutoweka kwa njia ya ajabu,  Mbwa wake akabaki ameinama kuficha uso wake,  muungurumo wa radi ulisikika kisha giza likatanda. 


Gafla Joker alionekana akiwa mbele ya jengo la hotel maandishi ya hotel yalisomeka "Gold Crest hotel" alitabasamu tena akatembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea Reception au Mapokezi Kama wanavyoita,  akiwa amevalia koti lake jeusi, chini akiwa amevaa mabuti makubwa meusi, mkononi Groves rangi nyeusi,  Nywele zikiwa bado kitimutimu,  alipokaribia kufika lango kuu la kuingia ndani,  walinzi walikaa tayari kusimama kwani mavazi aliyovaa yalionekana kuwa ya kiarifu, waliweka tayari bunduki zao na mara Gafla,  the Joker au Nyoka Mtu alibadilika na kuonekana kijana mtanashati aliyevalia Suti nyeusi nadhifu,  hali iliyofanya walinzi wabaki wamepigwa na butwaa na kutoamini walichokiona, The Joker aliwapita huku akitabasamu hadi mapokezi,  huku nyuma walinzi wakiongea " hizi Pombe za kunywa kabla hautajaingia lindo tuziache" masikio ya Joker yalisikia vizuri walichozungumza walinzi wale,  kana kwamba wamemwambia wakiwa wapo nae,  Joker akatabasamu tena na tayari alikua amefika kwa muhudumu wa mapokezi " Habari yako?" Alimsalimia,  "safi tu, karibu" "Asante" bila kupoteza muda Joker akamwambia, naelekea chumba namba 9, Mhudumu alinyanyua Simu ili apige mara Joker alimshika mkono,  binti aliporudisha macho kwa Joker hakuamini alichokiona, kwani alimuona kijana mzuri na mtanashati aliyesimama mbele yake,  akssita kisha kwa upole akamwambia "Nenda tu kaka",  The Joker Bila kupoteza muda akaelekea zilipo lift za hotel ile,  akabonyeza kitufe cha kufungua, kisha mlango ulipofunguka akaingia ndani ya lifti na Gafla akabadilika tena na kuonekana akiwa amevalia lile lile koti lake jeusi na mabuti Kama alivyoonekana akiwa anaingia hotelini..... 


JE KITATOKEA NINI!!?? USIACHE KUFATILIA SEHEMU YA PILI YA THE JOKER (Muuaji wa Siri)

Comments

Popular posts from this blog

SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza

SIMULIZI : Aisha Toka Tanga sehemu ya Pili

JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?