SIMULIZI : Aisha Toka Tanga sehemu ya Pili

Juma lililopita tuliona, Aisha akiwa amepata hifadhi katika bweni la wanafunzi la wavulana alipoingia chumbani na alipopanda tu kitandani akajikuta usingizi umempitia sasa endelea..............

Nikiwa nimesimama nje nikijiuliza jinsi nilivyofanya maamuzi ya gafla! Bila kufikiria, mara nilishtushwa na sauti ya mlinzi "Hussein!!!" nikageuka na kuangalia nyuma yangu, aha Mzee nilimuita, huyu mzee nilimfahamu nilipofika tu chuoni, tulitokea kijiji kimoja, na alinipokea na kunisaidia kujua mazingira ya chuo kabla hata sijapata marafiki,  ambao ni wanavyuo wenzangu, nilimuita Mzee sababu alipendwa kuitwa ivyo ingawaje umri wake haukua mkubwa sana alionekana ana umri Kati ya miaka 40 au 45 hivi.

Mbona umesimama mwenyewe hapa", aliniuliza, nilibaki kumshangaa sababu sikujua kama ataniuliza swali hilo, mara nyingi alizoea utani, pia nilishtushwa kumuona, sikupenda ajue kama ndani kwangu Kuna mgeni tena mgeni ambae ni wa kike,  sababu hajawahi kuniona nikiwa nimesimama na wasichana, nae alikua ni mmoja wa watu walio nisisitiza sana swala la kusoma.

"Nina mawazo tu mzee, nilimjibu nikiwa na wasiwasi " mawazo ya nini? " Ina maana leo huendi kula? Aliniuliza, Hapana nitaenda kula, kwani sasa hivi saa ngapi?" akiwa ameshika rungu lake mkononi akainama na kuangalia saa yake, sasa hivi ni saa mbili kasoro, umechelewa kula..." Aisee nimechelewa kweli, ngoja ni kachukue chakula nirudi kujisomea nilimwambia Mzee" akacheka na kama Kawaida yake akanitania tena " Leo ungelala njaa Shubamitt😀" nilicheka nikageuza haraka kurudi chumbani kwanza.

"Mjomba usisahau sigara zangu" Mzee aliniambia nikamuonyesha ishara ya poa, nilipofika mlangoni nilisikia sauti ndani kama mtu anapanga vitu, mlio wa Mfuko wa plastiki ulisikika kutoka ndani, nikafungua mlango taratibu, kweli nilimuona Aisha akiweka Mfuko mweusi katika moja ya begi lake, akanyanyuka akageuka na kuniangalia, nikiwa namalizia kufunga mlango alinikimbilia na kunikumbatia, sikuamini Kisha akasema,  "Hussein una roho nzuri sana" nilibaki nimeshangaa amelijua vipi jina langu la Hussein, maana umbali niliokuwepo, Mzee a kaniita,  na Yeye alipo ni mbali sana aliwezaje kusikia?. Akili yangu ikapuuza nilichokua nawaza nikabaki nimesimama na kumwangalia tu.

Aisha " naenda kuchukua chakula, utakula wali na maharage? Nilimuuliza" akaniangalia na kucheka sikujua anachekea nini "Ndio naweza kula" Kisha akatabasamu, " nikajikuta nasema" unajua nyie watoto wa kike mnapenda chips ku.... " kabla sijamaliza kusema akaniziba mdomo," nenda kalete chakula alisema. " nikaitikia kwa kutikisa kichwa kuashiria sawa,  " ila itabidi nifunge huu mlango kwa nje, nilimwambia "Sawa" alikubali, usinifikirie vibaya maana anaweza kuja mtu akafungua akikukuta itakua tatizo "usijali nimekuelewa". Nilivaa suruali na tisheti nyingine,  Nikatoka na kufunga mlango kwa nje.

Nikatembea na kuelekea ilipo kantini ya chakula, kwa Kawaida huwa nakula kwa bili,  na siku hiyo ratiba ilikua ni wali maharage, nikiwa nawaza usiku wa kwanza nitalala na msichana katika bweni la chumba chetu nilikua bado siamini, nikafika kantini na kuchukua sahani, nikapanga foleni kuelekea kwenye chakula, hapakua na wanafunzi wengi sana kama ilivyozoeleka siku zote, nilifika katika meza ya chakula na kumkuta mama Mosha, alizoea kuniita "Niyonzima ", aliponiona akatabasamu "umefika, ungechelewa kuja leo ungekuta ukoko tu," aliniambia huku akinipakulia chakula nilibaki kucheka nikamwambia aniwekee wali mwingi maana nina sikia njaa kweli, kumbe Moyoni mwangu nilikua najua kinachoendelea, ugeni ulinifanya niseme uongo bila kupenda," ndizi za kuiva zimeisha leo umechelewa," Mama Mosha alinitania, na mimi sahani yako nakuletea kesho nilimjibu, nikamuaga na kurudi na chakula changu bwenini.

Nikiwa nimekaribia kufika katika bweni, nikakumbuka sigara za mzee, " nikapita katika kiduka kidogo na kununua sigara aina ya "Faru" za Tsh Mia 200 na mfuko wa lailoni nikafunika chakula na kurudi bwenini, tayari ilikua imekaribia saa tatu usiku, nilifika getini na kumkuta Mzee amejifungia katika kibanda chake, Mzee, Mzee, Mzee?? Nilimuita akatoka "Aha umerudi" nikatoa sigara na kumpa, Kisha nikamuaga akili yangu yote ilikua kwa Aisha,  "asante Sana,  haya usiku mwema" nilimjibu.

Taratibu nikitembea katika korido ya bwenini, palikua kimya, nikiwa nimeshikilia chakula changu mkononi, nikafika katika mlango na kufungua taratibu, nikijua Aisha atakua amelala "He!!!! Aisha hakuwepo chumbani.... Nilipatwa na mshtuko nikajikuta naweka sahani mezeni kwa kuiangusha, nikainama chini ya uvungu wa kitanda Aisha hakuwepo nikabaki nashangaa," he hata mabegi yake pia Hayapo!!! Nikiwa nimepigwa na butwaa nikakurupuka kwa kukimbia hadi nje............

JE kimetokea nini?? AISHA AMEKWENDA WAPI................ USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA TATU HAPA SIKU YA JUMATANO.

Imeandikwa Na:
Daudi Mwidima (DM)

Namba: 0656 33 74 39 au 0754 542 642

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza

JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?