MAANA YA NDOTO MBAYA : NIGHTMARE

Nadhani wengi wenu mmewahi kusikia kuhusu Ndoto mbaya au Ndoto za kutisha, leo katika blog hii, tuta angalia kwa kina nini hasa usababisha ndoto mbaya au kama inavyojulikana kwa lugha ya kiingereza "nightmare"

Ndoto Mbaya ni nini? - hili ni swali linaloweza kujibiwa na mtu yoyote aliyepitia ama kuota ndoto mbaya, wapo watu wanafananisha ndoto mbaya na Nguvu za giza, yaani uchawi, wapo wengine wana amini ndoto mbaya zinatokana na ishara toka kwa mungu, hawa ni wale wanao amini kwa mungu, wapo wanao amini ndoto mbaya zinatokana na mizimu (marehemu), pia wapo wanaosema ndoto mbaya zinatokana na matendo ya mtu mwenyewe yaani kama mtu anafanya matendo mabaya, basi pia mtu huyo lazima ataota ndoto mbaya.

Hizo ni imani mbali mbali za watu tofauti kutokana na utafsiri wao katika ndoto, siwezi kusema wapo sahihi au hapana ila kwa sasa tuangalie kitu gani kinachosababisha ndoto mbaya/ nightmare.

Chanzo cha ndoto mbaya:
Tafiti mbali mbali, kuhusu mwili wa Binadamu zinaonyesha kua ndoto mbaya hutokea tu, pale mwili wa Binadamu unapoitaji msaada wa haraka pindi unapokua usingizini, dharula ya mwili kwa wakati huo inaweza kusababisha mwili kumfanya mtu kuota ndoto mbaya, tukumbuke mwili wa Binadamu pia umeumbwa na umeme wa asili, wengine watashangaa kusikia neno "umeme" ni kweli kabisa mwili wa Binadamu una umeme wa asili ndio maana watafiti mbali mbali kama Dr. Sebi kwa sasa ni marehemu, aliwahi kusema "human body produce enough electricity if such human eat organic foods" akasisitiza ulaji mzuri wa mboga mboga, samaki pamoja na matunda hufanya mwili kuchelewa kuzeeka na kua na Nguvu tofauti na mtu anaekula nyama nyekundu au vyakula vilivyolala (vyakula vyenye exipire date), nguvu anayozungumzia Dr. Sebi hapa ni umeme wa asili katika mwili wa Binadamu (nishati hai au nishati ya asili).

Sasa nirudi kwenye mada yenyewe ya chanzo cha ndoto mbaya, kama nilivyosema hapo juu sababu ya ndoto mbaya ni mwili kuitaji msaada wa haraka ukiwa usingizini Je? Msaada huu ni upi? Zifuatazo ni sababu baadhi ya Mtu kuota ndoto mbaya:


  • Mgandamizo wa hewa unaoenda  kwenye mapafu kua mdogo, husababisha Hali ya mtu aliyelala kuhisi kama ana kabwa na mtu au kitu kizito, ivyo mhusika atajikuta anaota mtu kaingia chumbani na kuanza kumkaba, lengo la ndoto mbaya nikuamsha mwili,  lli ulale katika Hali ya mapafu kupata hewa Safi, ivyo hali hiyo huisha mtu akifungua madirisha kama alikua kafunga madirisha nk.                     
  • Ulalaji mmbaya, Mwili kujifinya au kujibana, hii hutokea katika sehemu mojawapo ya kiungo mfano, mkono, mguu, au shingo nayo hupelekea mtu kuota ndoto mbaya, mfano mtu anaweza kuota anakabwa na mtu, au kaingiza mkono katika kitu ama sehemu inayokandamiza mkono au mguu wake, hali hiyo ya kuota huisha mtu huyo akibadilisha mlalo wake wa kulala.                                                              
  • Hali ya uchafu na vitu kua vingi chumbani, katika chumba cha kulala hakupaswi kua na vitu vingi, usingizi ni starehe sababu nusu ya maisha ya mwadamu ni usingizi - hii nayo inaweza kua sababu ya mtu kuota ndoto ya kutisha, mfano chumba kimejaa vitu ambavyo vilipaswa kua stoo kama vile jembe, fyekeo, pipa, nk, pia chumba kikiwa kichafu kuota unafukuzwa au unaliwa vidole na panya au unapapaswa na mtu ni hali ya kawaida sababu ya uchafu uliopo, shuka likiwa chafu hadi kufikia hatua ya kua na chawa tegemea kuota unapakwa upupu nk, pia vitu vikiwa vingi chumbani tegemea kuota taswira ya vitu hivyo pindi unapolala mfano ukilala, taswira ya mwisho katika macho yako iliona Jembe au kisu tegemea pia kuota ndoto inayoendana na kitu hicho. 
Makala hii itaendelea hapa ................... 

Imeandaliwa na Daudi Mwidima (DM) 2017.





Comments

  1. I want ndoto mbaya ya kutisha ni nini

    ReplyDelete
  2. Kuna ndoto na hii ni mara ya pili naota then nikiwa ndotoni kukimbia tatizo yaani nakua mzito sana

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza

SIMULIZI : Aisha Toka Tanga sehemu ya Pili

JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?