Mc Pilipili Apata Ajali Shinyanga
Mchekeshaji na mtumbuizaji katika sherehe, Immanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili, siku ya jana akiwa anaendesha gari aina ya Land Cruser rangi ya Silver, amepata ajali kijiji cha Bubiki/kata ya Mondo mkoa wa shinyanga baada ya kujaribu kumkwepa mtoto aliekua akikatiza barabarani na baiskeli, na kukimbizwa hospitali Bugando Jijini Mwanza.
Afisa uhusiano wa hospitali ya Bugando Lucy Joseph amekiri kumpokea Mc Pilipili na anashughulikiwa katika kitengo cha dharula hospitalini hapo.
Mc Pilipili alikua akitokea Jijini Mwanza kurudi Dar es salaam, kusherehesha sherehe, kamanda mkuu wa mkoa Shinyanga Simon Haule amekiri kutokea kwa ajali hiyo.

Comments
Post a Comment