Juma lililopita tuliona, Aisha akiwa amepata hifadhi katika bweni la wanafunzi la wavulana alipoingia chumbani na alipopanda tu kitandani akajikuta usingizi umempitia sasa endelea.............. Nikiwa nimesimama nje nikijiuliza jinsi nilivyofanya maamuzi ya gafla! Bila kufikiria, mara nilishtushwa na sauti ya mlinzi "Hussein!!!" nikageuka na kuangalia nyuma yangu, aha Mzee nilimuita, huyu mzee nilimfahamu nilipofika tu chuoni, tulitokea kijiji kimoja, na alinipokea na kunisaidia kujua mazingira ya chuo kabla hata sijapata marafiki, ambao ni wanavyuo wenzangu, nilimuita Mzee sababu alipendwa kuitwa ivyo ingawaje umri wake haukua mkubwa sana alionekana ana umri Kati ya miaka 40 au 45 hivi. Mbona umesimama mwenyewe hapa", aliniuliza, nilibaki kumshangaa sababu sikujua kama ataniuliza swali hilo, mara nyingi alizoea utani, pia nilishtushwa kumuona, sikupenda ajue kama ndani kwangu Kuna mgeni tena mgeni ambae ni wa kike, sababu hajawahi kuniona nikiwa nimesimama na wa...
Comments
Post a Comment