Kutoka kushoto ni Mh. Lomu, Msigwa, Mke wa Lissu, Mbowe, Kubenea, Mh Lema na mwenye suruali nyekundu ni dereva wa Tundu Lissu wakiwa katika picha ya pamoja Jijini Nairobi.
Nakumbuka ilikua ni siku ya jumamosi nikiwa nimemaliza kufanya mazoezi ya kukimbia, katika kiwanja cha chuo kikuu Jijini Dar es salaam, kwa Kawaida huwa napenda sana kufanya mazoezi siku ya jumamosi, nizunguke Uwanja mara kumi na tano hadi ishirini, Kisha baada ya hapo narudi bwenini kwa ajili ya kuoga na kujiandaa kwenda katika madarasa kwa ajili ya kujisomea. Nikiwa mwanafunzi wa Ualimu katika kitivo cha Elimu, mwaka wa pili, chuoni hapo, na toka nifike chuoni sikupenda kua na marafiki, ivyo nilikua naishi maisha ya kujitenga na wanafunzi wenzangu muda wote, rafiki yangu mkubwa ilikua ni Elimu na mazoezi na kila nilikua nikifikiria hali ya kimaisha nyumbani jinsi ilivyo duni, niliona ni bora nisome kwa bidii ili nije kuwasaidia nyumbani. Sikupenda kabisa kua na marafiki, maana niliogopa wanaweza kunivurugia ndoto zangu za kufikia malengo yangu. Nikiwa bado na hema kwa nguvu kutokana na kumaliza kukimbia gafla!! Mvua ilianza kunyesha nikiwa nipo kifua wazi nimevaa bukta...
Juma lililopita tuliona, Aisha akiwa amepata hifadhi katika bweni la wanafunzi la wavulana alipoingia chumbani na alipopanda tu kitandani akajikuta usingizi umempitia sasa endelea.............. Nikiwa nimesimama nje nikijiuliza jinsi nilivyofanya maamuzi ya gafla! Bila kufikiria, mara nilishtushwa na sauti ya mlinzi "Hussein!!!" nikageuka na kuangalia nyuma yangu, aha Mzee nilimuita, huyu mzee nilimfahamu nilipofika tu chuoni, tulitokea kijiji kimoja, na alinipokea na kunisaidia kujua mazingira ya chuo kabla hata sijapata marafiki, ambao ni wanavyuo wenzangu, nilimuita Mzee sababu alipendwa kuitwa ivyo ingawaje umri wake haukua mkubwa sana alionekana ana umri Kati ya miaka 40 au 45 hivi. Mbona umesimama mwenyewe hapa", aliniuliza, nilibaki kumshangaa sababu sikujua kama ataniuliza swali hilo, mara nyingi alizoea utani, pia nilishtushwa kumuona, sikupenda ajue kama ndani kwangu Kuna mgeni tena mgeni ambae ni wa kike, sababu hajawahi kuniona nikiwa nimesimama na wa...
Hili linaweza kuonekena kama kichekesho au mshangao, kwa watu wengine haswa kwa wale ambao kipato Chao ni cha kawaida au cha Kati, ila kwa matajiri wapenda starehe jambo hili Kwao ni la kawaida kabisa, waswahili wanasema, "ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauni" sasa ungana na mimi kujua baadhi ya Pombe nikimaanisha aina yoyote ya kilevi iwe wine, wisky, grants, beer n.k zenye bei kubwa Duniani. Hii ni Richebourg Grand Chuck, iliyotengenezwa na Henry Jayer miaka ya 1978, bei yake kwa thamani ya kitanzania ni Milioni 47!!!! Hahaha najua unashangaa maana milioni 47 kwa Tanzania inatosha kabisa kujenga nyumba ya kawaida na kununua gari ndogo ya kutembelea. Tukiachana na Richebourg Grand Chuck ambayo ndugu msomaji, unaweza kubisha kua haiuzwi bei hiyo, basi ngoja nikuletee aina nyingine ya Pombe hii imeandikwa hadi lebo ya bei kwa thamani ya pesa za kitanzania nayo ni hii hapa: Hennessy, ikiwa na Lebo iliyoandikwa Milioni 2 na laki 5 za kit...
Comments
Post a Comment