Leo Katika Burudani - Vitali Maembe
Leo Katika Burudani, tunae Vitali Maembe, msanii kijana toka Bagamoyo, maarufu kwa wimbo wa "Sumu ya teja" wengi ukitaja wimbo huo wanaweza kua wanajua wimbo huo, bila kumjua msanii mwenyewe, hii inatokana na msanii huyu kupendelea zaidi kuimba nyimbo za jukwaani, ijapokua ana video kadhaa kama wimbo wa Katiba ambao ameshautolea video.
Aina ya nyimbo zake ni kuhamasisha watu, kuipenda nchi yao ya Tanzania, kujitambua, kuhimiza utawala bora na mambo mengine yanayohusu maadili ya Mtanzania, baadhi ya nyimbo alizokwisha toa ni KUDU, VUMA, pamoja na KATIBA.
Uwezo wake katika kupiga Gitaa akiwa anaimba ndio uliompa zaidi umaarufu, inasikitisha kwa upande mwingine wasanii wazuri kama Hawa kutowasikia tena na tukiacha wakipotea na nyimbo zao zenye mvuto katika kusikiliza na kujifunza.
Nikipata kibali toka kwake nitaweka baadhi ya nyimbo zake hapa ili wengi wetu tupate kumjua zaidi.
Makala hii imeandaliwa na
Daudi Mwidima

Comments
Post a Comment