JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?
Hili linaweza kuonekena kama kichekesho au mshangao, kwa watu wengine haswa kwa wale ambao kipato Chao ni cha kawaida au cha Kati, ila kwa matajiri wapenda starehe jambo hili Kwao ni la kawaida kabisa, waswahili wanasema, "ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauni" sasa ungana na mimi kujua baadhi ya Pombe nikimaanisha aina yoyote ya kilevi iwe wine, wisky, grants, beer n.k zenye bei kubwa Duniani.
Hii ni Richebourg Grand Chuck, iliyotengenezwa na Henry Jayer miaka ya 1978, bei yake kwa thamani ya kitanzania ni Milioni 47!!!! Hahaha najua unashangaa maana milioni 47 kwa Tanzania inatosha kabisa kujenga nyumba ya kawaida na kununua gari ndogo ya kutembelea.
Tukiachana na Richebourg Grand Chuck ambayo ndugu msomaji, unaweza kubisha kua haiuzwi bei hiyo, basi ngoja nikuletee aina nyingine ya Pombe hii imeandikwa hadi lebo ya bei kwa thamani ya pesa za kitanzania nayo ni hii hapa:

Hennessy, ikiwa na Lebo iliyoandikwa Milioni 2 na laki 5 za kitanzania, fedha ambayo inatosha kabisa kulipia Ada ya chuo kikuu kwa mwaka mzima au mtaji wa kuanzisha biashara.
Comments
Post a Comment