Mh. KASSIM MAJALIWA - Thamani ya Dhahabu Nyeupe irudi
Waziri mkuu wa Tanzania, mh. Kassim Majaliwa akiwa mjini Dodoma alifanya mkutano na wakuu wa mikoa inayoongoza kuzalisha zao la Pamba, ikiwemo mkoa wa Mara, Mwanza, Simiyu, Morogoro, Shinyanga pamoja na singida.
Katika mkutano huo waziri Mkuu kassim Majaliwa, aliwataka wa kuu wa mikoa hiyo kua na Agenda moja ya kuinua kwa pamoja zao la Pamba ambalo lilijulikana kama "Dhahabu Nyeupe", sifa ambayo ilipotea baada ya changamoto ya nguo kutoka nchi za nje, pamoja na Mabadiliko ya Hali hewa pamoja na kitekinolojia.
Kama ambavyo serikali ya Awamu ya tano ya Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli, ikisisitiza kuhusu "uchumi wa viwanda", jitahada izo za kuinua uchumi zinaenda pamoja na kuinua kilimo haswa zao la biashara ambalo tayari lilikua limeanza kupotea.
Waziri mkuu pia alisisitiza kuhusu utaratibu wa kuinua zao hilo, lazima uanzie katika utaratibu wa kuchagua mbegu bora, matayarisho ya shamba hadi kufikia hatua ya kuvunwa na kuuzwa. "lazima kila mkoa uwe na afisa kilimo bora" alisisitiza.
Ufufuaji huo wa Pamba utaenda pamoja na kuinua upya zao la Chai, Kahawa pamoja na Alizeti.

Comments
Post a Comment