NDOTO MBAYA - NIGHTMARE sehemu ya 2

Katika makala yaliyopita, tuliona jinsi ambavyo mtu anaweza kujikuta anaota ndoto mbaya, (bad dream) au nightmare, kutokana na mazingira ya chumba alicholala, niligusia vitu baadhi ikiwemo chumba kutokua kisafi, kujaza vitu vingi chumbani nk, sasa endelea........

Sababu ya tatu ya mtu kujikuta anaota ndoto mbaya, inaweza kusababishwa na matukio ya kimaisha, ya kila siku hapa nitagawa matukio ya kimaisha katika pande kuu mbili (2) :
(1) Aina ya Kazi
(2)Aina ya mazingira

Aina ya kazi - hii inaweza kua chanzo cha mtu kuota ndoto mbaya pindi aingiapo kulala, mfano, mtu anafanya kazi ya mochwari mara nyingi anajikuta anahusika na kutunza miili ya marehemu, hii hupelekea mtu huyo kuota ndoto mbaya,  anaweza kujikuta anaota,  aidha amekaa na marehemu nk. Hali hii pia huwatokea watu wanaofanya kazi katika maeneo hatarishi, kama katika majengo marefu, anaweza kuota anadondoka nk, au mitambo mikubwa ya viwandani nk.

Tukumbuke ubongo wa Binadamu una tabia ya kupokea kila kitu unachokiona , na inapotokea mtu huyo anawaza sana aidha kitu fulani kwa muda mrefu, Hali hiyo pia inaweza kujirudia kwenye ndoto kwa namna yoyote ile iwe nzuri au mbaya.

Aina za mazingira, kuna baadhi ya watu wanaishi katika mazingira ambayo ikifika muda wa usiku mazingira yao, yanatisha,  yaani ikifika saa moja usiku tu, mtu unaogopa kutoka nje na hofu inakua,  kubwa zaidi Choo kikiwa cha nje mfano vijijini, unaweza kukuta mtu anaogopa hadi kutoka nje, Hali hii ya wasiwasi tukumbuke huwa haiishi katika kuogopa tu bali inabaki katika Fikra ya mtu hadi muda ambao mtu huyo anaingia kulala inaweza kuendelea nakujikuta anaishia kuota ndoto ya kutisha, pia kuishi katika nyumba ambayo mbele Kuna makaburi, miti mingi au giza nene, kunaweza kusababisha hali hii.

Nini ufanye usiote Ndoto mbaya..?

Kwanza hakikisha, kabla ya kulala unaangalia vitu vinavyopendeza macho yako na akili yako au kusikiliza simulizi nzuri za kuvutia au kuchekesha au kutizama picha nzuri unazopenda.

Pili, safisha chumba chako cha kulala, kiwe Safi, fua mashuka, Pazia za madirishani, safisha uvungu wa kitanda na sehemu nyingine, hakikisha unapata hewa Safi chumbani.

Tatu, Epuka kutumia shuka zenye rangi Nyeusi, nyekundu (hili nitalifafanua siku za usoni)

Nne, kazi ya chumba ni kulala Epuka kuweka vitu vingi chumbani kama ndoo za maji, vifaa vya kilimo kama majembe nk. Na kama huwezi kabisa basi hakikisha unatafuta kitambaa cheupe ufunike vitu hivyo kabla ya kuingia kulala.

Tano, Panda kitandani ukiwa umeoga hakikisha mwili wako ni msafi kabla ya kuingia kulala.

Sita, kabla ya kulala jipe muda wa kutafakari mambo mazuri ya kimaisha, jitabilie ushindi, jisifie kua wewe unaweza, jikubali. jilazimishe kutabasamu ata kama una mawazo au mambo magumu yanakutatiza usisahau pia kusali kwa imani yako.

Saba, Epuka kula hadi kufikia hatua ya kuvimbiwa, wakati wa kulala usile vyakula vigumu ambavyo umeng'enyaji wake wa chakula huchukua muda mrefu na kama ikitokea umekula hivyo basi hakikisha unakunywa maji mengi kabla ya kulala hii itasaidia katika kulainisha chakula.

Fanya ivyo na ndoto mbaya zitakua historia kwako, Tukumbuke hakuna Uchawi unaotumwa mtu kuota ndoto mbaya ni SISI WENYEWE.

Kama umefanya yote hayo na Hali ya kuota ndoto mbaya bado inaendelea Wasiliana na mimi kupitia: +255656 33 74 39 au +255754 542 642 au B arua Pepe:daudimwidima09@gmail.com

Makala hii imeandikwa Na: Daudi Mwidima (DM). 2017

Comments

Popular posts from this blog

SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza

SIMULIZI : Aisha Toka Tanga sehemu ya Pili

JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?