SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza
Nakumbuka ilikua ni siku ya jumamosi nikiwa nimemaliza kufanya mazoezi ya kukimbia, katika kiwanja cha chuo kikuu Jijini Dar es salaam, kwa Kawaida huwa napenda sana kufanya mazoezi siku ya jumamosi, nizunguke Uwanja mara kumi na tano hadi ishirini, Kisha baada ya hapo narudi bwenini kwa ajili ya kuoga na kujiandaa kwenda katika madarasa kwa ajili ya kujisomea. Nikiwa mwanafunzi wa Ualimu katika kitivo cha Elimu, mwaka wa pili, chuoni hapo, na toka nifike chuoni sikupenda kua na marafiki, ivyo nilikua naishi maisha ya kujitenga na wanafunzi wenzangu muda wote, rafiki yangu mkubwa ilikua ni Elimu na mazoezi na kila nilikua nikifikiria hali ya kimaisha nyumbani jinsi ilivyo duni, niliona ni bora nisome kwa bidii ili nije kuwasaidia nyumbani. Sikupenda kabisa kua na marafiki, maana niliogopa wanaweza kunivurugia ndoto zangu za kufikia malengo yangu. Nikiwa bado na hema kwa nguvu kutokana na kumaliza kukimbia gafla!! Mvua ilianza kunyesha nikiwa nipo kifua wazi nimevaa bukta...
Comments
Post a Comment