SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza
Nakumbuka ilikua ni siku ya jumamosi nikiwa nimemaliza kufanya mazoezi ya kukimbia, katika kiwanja cha chuo kikuu Jijini Dar es salaam, kwa Kawaida huwa napenda sana kufanya mazoezi siku ya jumamosi, nizunguke Uwanja mara kumi na tano hadi ishirini, Kisha baada ya hapo narudi bwenini kwa ajili ya kuoga na kujiandaa kwenda katika madarasa kwa ajili ya kujisomea. Nikiwa mwanafunzi wa Ualimu katika kitivo cha Elimu, mwaka wa pili, chuoni hapo, na toka nifike chuoni sikupenda kua na marafiki, ivyo nilikua naishi maisha ya kujitenga na wanafunzi wenzangu muda wote, rafiki yangu mkubwa ilikua ni Elimu na mazoezi na kila nilikua nikifikiria hali ya kimaisha nyumbani jinsi ilivyo duni, niliona ni bora nisome kwa bidii ili nije kuwasaidia nyumbani.
Sikupenda kabisa kua na marafiki, maana niliogopa wanaweza kunivurugia ndoto zangu za kufikia malengo yangu. Nikiwa bado na hema kwa nguvu kutokana na kumaliza kukimbia gafla!! Mvua ilianza kunyesha nikiwa nipo kifua wazi nimevaa bukta rangi nyeusi ya mpira pembeni ikiwa imeandikwa 'Sport lite' , nilitembea hatua kadhaa na kwenda kuchukua begi langu pembeni ya nguzo ya gori nikaanza kukimbia taratibu kuelekea lilipo bweni letu la wanafunzi wa kiume.
Nilivuka majengo kadhaa mvua ikiwa inaendelea kunyesha, nilipofika katika korido kubwa ambako juu yake, kumezibwa na Paa, nilitoa taulo katika begi nikaanza kujifuta maji usoni huku nikipiga hatua kadhaa, nikiwa nimefika usawa wa kukaribia bweni letu, Gafla nilisikia sauti ya mtu akilia, akili yangu ikaniambia geuka uangalie, kugeuza kichwa nilimuona Dada mmoja akiwa na begi kubwa la nguo pamoja na begi dogo la mgongoni akiwa kajiinamia chini analia huku akiwa amelalia begi lake dogo.
Haraka nikajiuliza huyu binti katokea wapi na mbona analia?, nilipomuangalia kwa umakini nikagundua atakua mwanafunzi pale chuoni, lakini sababu wanafunzi wapo wengi huwezi kujua wanafunzi wote "lazima kutakuwa na jambo yawezekana amefiwa?" nilibaki kujiuliza lakini kama ninavyojijua huwa sijipi muda sana na watu nikataka kupiga hatua kuendelea na safari yangu ya kurudi bwenini.... Wakati nainua mguu, Yule binti aliniita kwa sauti ya kigugumizi "we.... we..!! Kaka!?" nikageuka kumwangalia "samahani na.. naomba unisaidie" binti akaniambia huku akiniangalia na kufuta machozi.
Huruma ikaniingia nikajikuta naenda alipokua amekaa huku nikitafuta tisheti katika kibegi changu na kuvaa, muda wote huo hakuna mtu yeyote aliyepita eneo lile "Ehe? Niambie dada...?" yule dada kwa aibu akageuka upande mwingine nakuanza tena kulia hali iliyonifanya niingiwe na huruma tena huruma ya kutaka kujua kitu gani kimempata msichana yule, nilipomuangalia haraka haraka alionekana ni binti mrembo, Rangi yake ya maji ya kunde na nywele zake za asili alizobana kwa nyuma zilimzidisha kuonekana mrembo.
Nikamuuliza "Umeniita una shida gani"? Akageuza kichwa na kuniangalia, huwezi amini ndugu msomaji sijawahi toka nizaliwe kuangaliana na binti macho kwa macho tena kwa ukaribu, nilijikuta nimezubaa, macho yake yalikua makubwa ya duara nilihisi kama Kuna sumaku ikinivuta nimsogelee,
nikakumbuka maneno ya rafiki yangu mmoja kijijini aliwahi kuniambia, wasichana wa chuo ni wazuri kama malaika nikiwa chuo niwe makini', kauli ile ilinizindua haraka nikajikuta narudi nyuma kidogo nikawa nimekaa chini kama wanavyokaa wachezaji wa mpira wakimsikiliza kocha wao.
Yule Dada alitoa simu yake aina ya smartphone akawa anaangalia Kisha akasema Kwa sauti ya chini "jamani mnanichanganya mimi sijui chochote" akaizima simu Kisha akiniangalia tena na kuniuliza "kaka unasoma hapa"? Nikamjibu "Ndio" huku nikiwa najua ataniuliza swali jingine nikawa tayari kumjibu, nikamuona anataka tena kulia, nikajikuta namshika bega nakumsihi asilie aniambie alichoniitia, akaniangalia na kuniuliza "Naweza kukuamini?, nilimjibu ndio akaniangalia kwa jicho la kuona kama ninachosema ni ndio au hapana,
Akaanza kunisimulia mkasa wake uliomkuta hadi kujikuta analia," Mimi naitwa Aisha ni mwanafunzi mwaka wa kwanza , kitivo cha Sheria... Nilikua nakaa na rafiki yangu wa kike nje ya eneo la chuo yaani (out of campus), toka nimefika chuo yeye ndie aliyenipokea kipindi tunafanya usaili wa kuanza chuo huyo dada alitokea tu kunizoea na mimi kumzoea nikamwambia sina mahali pa kufikia na nyumbani bado hawajanitumia pesa ya kutafuta hosteli nina pesa kidogo tu ya kulala nyumba za wageni, na chuo hawana msaada, yule dada alinionea huruma, (Aisha akaanza kulia tena) ni kafanya kazi nyingine ya ziada kummbeleza, akanyamaza na kuendelea.......
"basi yule dada akanionea Huruma akasema yeye ana sehemu yake twende tukaishi wote, sasa leo nimeshangaa anakuja na mwanaume nikiwa nimelala akaniambia nitoke nitafte sehemu nyingine ya kukaa, huku akilalamikia tabia yangu kua usiku silali nawasha taa nasoma usiku mzima, yeye hapati usingizi akiwa amelala, nilijaribu kumbembeleza anipe muda akanikatalia namimi sina rafiki mwingine hapa chuoni ni mgeni, Aisha akaanza tena kulia.
Nikiwa nawaza jinsi ya kumsaidia, maana katika chumba changu tupo watu wawili mwenzangu mmoja alikua kasafiri baada ya kupata msiba wa mama yake, mara walipita wanafunzi wengine walipotuona wakanitania "aha Hussein tunakuona leo umeopoa" huku wakicheka na kuondoka zao sikuwajali.
Nikamuuliza Aisha "ulitaka nikusaidie nini ?" Aisha alianza tena kulia, nikajikuta nanyanyuka namshika mkono na kumnyanyua nae akakubali Kisha nikachukua begi lake moja na kumsaidia hadi katika bweni langu, tulipofika tu Aisha alivua Viatu nakujitupa kitandani hapo hapo akapitiwa na usingizi nikiwa bado najishangaa kwa Uamuzi wa gafla! Niliochukua nikatoka nje, nakuanza kujiuliza Je walinzi wakipita usiku itakuaje?? Na je rafiki yangu akirudi pia itakuaje? Kha!! Ninafanya nini Hussein, nilijiuliza,..........
JE? Kitatokea nini? Usikose kufatilia sehemu ya Pili hapa......... Siku ya Jumatano.
Imeandikwa Na: Daudi Mwidima (DM)
2017.

Comments
Post a Comment