MCHUNGAJI GWAJIMA KUMUOMBEA TUNDU LISSU
Siku ya Jana tarehe 8/09/2017, mchungaji Joseph Gwajima, alitangaza kufanya maombi maalum, kumuombea mwanasheria mkuu wa Chadema ambae, pia ni Rais wa Tanganyika law society (TLS) Tundu Antipas Lissu, aliyejeruhiwa kwa kupigwa Risasi mjini Dodoma siku ya tarehe 7/09/2017 Alhamisi na watu wasiojulikana na kukimbizwa hospitali ya Dodoma na baadae kusafirishwa na ndege ya Dharula kwenda nchini Kenya, Nairobi katika hospitali ya Aga - khan kwa matibabu zaidi, maombi hayo yatafanyika kanisani kwake, Ubungo maarufu kama kanisa la ufufuo na uzima.
Mchungaji Joseph Gwajima ni mmoja ya wachungaji nchini Tanzania anaefuatilia kwa umakini mkubwa Hali ya kisiasa Tanzania na kukemea na kuonya pale inapobidi Hali inayopelekea kugongana na vyombo vya dola mara kwa mara.
Hali ya sasa Tanzania inatisha jeshi la polisi linapaswa kufutilia na kuhakikisha wahusika wote wanapatikana
ReplyDelete