BURUDANI : JE? UNAMJUA DJ KHALED Hii ni historia yake fupi



DJ Khaled, wengi humtambua kwa jina hilo ila jina lake halisi ni "Khaled Mohammed  Khaled" alizaliwa November 26, 1975 bila shaka umri wake utakua miaka 42 hivi sasa, kabla ya kuitwa DJ Khaled alijulikana kwa majina tofauti tofauti kama vile, "Beat Novacana, na Arab Attack, jina la Arab attack aliamua kulibadilisha baada ya kutokea kwa shambulio la kigaidi la tarehe 9/11/2001,  nchini marekani.

DJ Khaled alianza shughuli za Muziki akiwa kama" DJ" na ndio sababu ya jina lake kuanzia na neno DJ, kazi ambayo kwa mujibu wa jarida la foxy,  alikiri kua anaipenda kazi hiyo hadi sasa, pia ni Rapper, song writer na sasa ni Producer, uwezo wake pia katika kucheza vifaa vya Muziki haupo nyuma anaweza kucheza vifaa mbali mbali ikiwemo kinanda, na guitar.

Tangu aanze Muziki alishapitia kampuni mbali mbali za kimuziki ikiwemo Young money, Cash money, pamoja na Def Jam south, lakini kwa sasa ana kampuni yake mwenyewe inayojulikana kwa title kubwa ya "Another One"

Mwaka huu 2017, ndio Mwaka ambao DJ Khaled ametokea kufanya vizuri katika ulimwengu wa Muziki kwa kuachia Album ya "GRATEFUL" iliyovunja rekodi ya Billboard, aliyoshirikisha wakali kadhaa wa Muziki ikiwemo Rihanna, Sizzla, Chris brown, Montana n.k na moja ya sifa kubwa inayompa sifa DJ Khaled ni uwezo wake wa kuleta wasanii pamoja katika wimbo ata kama wasanii hao hawapatani.

Katika upande wa mahusiano DJ Khaled,  hayupo wazi sana kama wasanii wengine lakini mwaka huu,  ni kama mwaka wake akitokea mara nyingi katika vyombo vya habari, akimuonyesha mwanae wa kiume "junior Khaled" zaidi katika  page yake ya instagram.
                   
           DJ khaled akiwa na mwanae

Comments

Popular posts from this blog

SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza

SIMULIZI : Aisha Toka Tanga sehemu ya Pili

JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?