Posts

Showing posts from 2020

The One Boy Group (Warembo na Watanashati

Image
Kutana na Kikundi cha One Boy Group (Warembo na Watanashati)  Na Daudi Mwidima:  Kikundi   hiki kinachoundwa na wasanii, wa maigizo,  Filamu pamoja na aina nyingine ya sanaa chenye maskani yake Mbagala Jijini Dar es salaam,  chenye Takribani Miezi Nane toka kuanzishwa kwake, kikiwa chini ya kiongozi wao "One boy" mwaka huu wa 2020 - 2021 kimejiwekea mikakati mbalimbali ya kisanii ikiwemo kuandaa Safari tour ya kuzunguka mikoa mbalimbali ya Nchini Tanzania lengo likiwa kutoa burudani na kuelimisha jamii kupitia kazi za sanaa wanazofanya, Pia kutoa video za maigizo pamoja na aina nyingine ya Filamu ambazo zitabeba maudhui ya uchekeshaji pamoja na kuelimisha jamii,  kupitia You tube channel na mitandao mingine ya kijamii.  Watanzania na nchi jirani sasa wakae mkao wa kula kupokea kazi za wasanii hawa ambao wamepania kuitikisa vilivyo sanaa ya bongo,  baada ya kufanya nao mahojiano nikiwa pamoja na Mkurugenzi wa kundi Mr.  One Boy na Msanii ...

SIMULIZI: THE JOKER - Muuaji wa Siri Sehemu ya kwanza hii Hapa

Image
 - THE JOKER (Muuaji wa Siri)  Sehemu ya Kwanza hii hapa: Katika Nchi ya Tanzania,  jijini Mwanza,  yapata saa tano za usiku, katikati mwa jiji la Mwanza eneo la Capri point,  mtaa wa sita kutoka barabara Kuu ya kuingia katika jengo la Benki Kuu ya Tanzania,  nyumba namba 43 nyumba ambayo geti lake lilikua la chuma kilichochakaa,  Upande wa ndani kulikua na nyasi nyingi zilizoonyesha hazijapata kufyekwa takribani miaka miwili, pembeni mwa jengo lile kulikua na gari bovu aina ya land Cruiser rangi ya bluu,   Lango la kuingilia ndani pembezoni kabisa mwa ukuta palikua na Pipa, ambalo ndani yake kulikua na karatasi zinaendelea kuwaka,  humo  ndimo alimojificha Joka Mtu,  au kwa jina lingine unaweza kumuita The Joker,  akiwa kasimama katika kioo kilichopasuka,  shingoni akiwa kajifunga mnyororo mrefu uliofika hadi kwenye kiuno kisha kurudi tena shingoni na kushuka hadi chini,  hakika ulionekana mnyororo mzito kwelikw...