The One Boy Group (Warembo na Watanashati

Kutana na Kikundi cha One Boy Group (Warembo na Watanashati) 

Na Daudi Mwidima: Kikundi   hiki kinachoundwa na wasanii, wa maigizo,  Filamu pamoja na aina nyingine ya sanaa chenye maskani yake Mbagala Jijini Dar es salaam,  chenye Takribani Miezi Nane toka kuanzishwa kwake, kikiwa chini ya kiongozi wao "One boy" mwaka huu wa 2020 - 2021 kimejiwekea mikakati mbalimbali ya kisanii ikiwemo kuandaa Safari tour ya kuzunguka mikoa mbalimbali ya Nchini Tanzania lengo likiwa kutoa burudani na kuelimisha jamii kupitia kazi za sanaa wanazofanya, Pia kutoa video za maigizo pamoja na aina nyingine ya Filamu ambazo zitabeba maudhui ya uchekeshaji pamoja na kuelimisha jamii,  kupitia You tube channel na mitandao mingine ya kijamii. 

Watanzania na nchi jirani sasa wakae mkao wa kula kupokea kazi za wasanii hawa ambao wamepania kuitikisa vilivyo sanaa ya bongo,  baada ya kufanya nao mahojiano nikiwa pamoja na Mkurugenzi wa kundi Mr.  One Boy na Msanii mwenzie Umber Linda ambae alikuja kuingia kwenye ugomvi na Msanii mwenzie Umber Ruty,  mengi kati yaliyotokea tutayasikia kupitia You tube channel, amesema watanzania  wawe tayari kupokea kazi mpya za wasanii na sio kuendelea kuangalia wasanii wale wale kila siku hivyo basi tuwape nafasi ili tuone kama Yaliyomo Yamo. 


Msanii One Boy akiwa kwenye Pozi la kisanii 


 Umber Linda akiwa Katika pozi matata la kisanii 


Comments

Popular posts from this blog

SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza

SIMULIZI : Aisha Toka Tanga sehemu ya Pili

JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?