SIMULIZI YA SIKU YA KWANZA KABURINI hii hapa
Habari!? Kwa jina naitwa John Sindano, Mzaliwa wa Mkoa wa Mwanza, kijiji cha Buhima kata ya Ukiriguru, kaskazini mwa nchi ya Tanzania pembezoni mwa ziwa maarufu barani afrika, ziwa lenye samaki watamu aina ya Sato na sangara, likifahamika kama ziwa Nyanza, kwa wakazi wa Mwanza na sehemu nyingine jirani ya Tanzania, lakini kidunia likijulikana kama ziwa Victoria, hii ni baada ya malkia wa uingereza Queen Victoria kutembelea eneo hilo la ziwa yapata miaka elfu moja mia nane na hamsini nane (1858) iliyopita, Nadhani wengi wenu mlishawahi kusikia simulizi ya ziwa hili Kama sio kuisoma katika historia, moja ya maajabu ya ziwa hili ni kwamba, ndio ziwa pekee linalopokea maji yake toka mto Nile, nchini Libya na maji hayo hutiririka miaka nenda rudi toka Libya hadi katika ziwa Victoria, Sikuja hapa kukuelezea kuhusu historia ya nchi yetu ya Tanzania, Bali Nimejikuta naeleza yote hayo, baada ya wewe ndugu yangu kunionyesha Ukarimu wa Hali ya juu, Ukarimu ambao unapatikana nc...