SIMULIZI YA SIKU YA KWANZA KABURINI hii hapa
Habari!? Kwa jina naitwa John Sindano, Mzaliwa wa
Mkoa wa Mwanza, kijiji cha Buhima kata ya Ukiriguru,
kaskazini mwa nchi ya Tanzania pembezoni mwa
ziwa maarufu barani afrika, ziwa lenye samaki watamu aina
ya Sato na sangara, likifahamika kama ziwa Nyanza, kwa
wakazi wa Mwanza na sehemu nyingine jirani ya Tanzania,
lakini kidunia likijulikana kama ziwa Victoria, hii ni baada
ya malkia wa uingereza Queen Victoria kutembelea eneo hilo
la ziwa yapata miaka elfu moja mia nane na hamsini nane
(1858) iliyopita, Nadhani wengi wenu mlishawahi kusikia
simulizi ya ziwa hili Kama sio kuisoma katika historia, moja ya
maajabu ya ziwa hili ni kwamba, ndio ziwa pekee linalopokea
maji yake toka mto Nile, nchini Libya na maji hayo hutiririka
miaka nenda rudi toka Libya hadi katika ziwa Victoria,
Sikuja hapa kukuelezea kuhusu historia ya nchi yetu
ya Tanzania, Bali Nimejikuta naeleza yote hayo, baada ya
wewe ndugu yangu kunionyesha Ukarimu wa Hali ya juu,
Ukarimu ambao unapatikana nchini Tanzania pekee, kama
sio Duniani kwa ujumla, hukujali mavazi yangu yaliyotatuka
wala mwonekano wa Hali yangu ya kimasikini, nilipobisha
hodi, Nilipokusalimu nawe bila hiyana uliitikia na kunisikiliza
shida yangu, hakika nilikuwa na kiu! Tena, kiu haswaa! Kiu
ambayo imechanganyika na maumivu ya kuumwa mwili
pamoja na akili, kiu isiyoweza kutulizwa hata na glasi hii ya
maji, walakini nimeyapata maji haya, japo ni kidogo nami
nitakunywa angalau nipoze kiu yangu, kiu ya kimwili itatulia,
lakini kiu ya haki yangu, jasho langu na muda wangu sidhani
kama itatulizwa na maji haya hadi siku niingiapo tena kaburini.
Kupata simulizi hii Kamili nipigie 0754542642 au 0656 337439
Comments
Post a Comment