BONGO WRITERS (UMOJA WA WAANDISHI WA VITABU) Vitabu ndio Mlezi wa Maendeleo

Dunia ikiwa inakimbizana na Maendeleo ya Sayansi na Tekinolojia, Haiwezi kuendelea mbele bila watu Kusoma vitabu na kupata maarifa ya kuweza kuwasaidia waweze kugundua vitu mbalimbali, na kufikia malengo makubwa ya kitekinolojia na kisayansi, Usomaji wa vitabu ndio sehemu Pekee ya binadamu kupanua mawazo yake na kufikia malengo anayayoyataka kimaendeleo iwe kiuchumi, kijamii hata kisiasa, Vitabu ni Mlezi wa maendeleo katika Nchi yoyote ile, tunaweza kusema Vitabu ndio "Mama wa maendeleo" kwani maarifa yote tunayotumia ili kuweza kupiga hatua za kimaendeleo, yamefichwa katika vitabu, Kuliona hilo Bongo Writer wamekuja na hili kusaidia na kuhamasisha usomaji wa vitabu Tanzania,

Bongo Writers (BW) ni nini? 

Bongo Writers ni Umoja wa waandishi wa Vitabu walioamua kuungana na kusimamia kazi zao kwa pamoja ikiwemo Kuuza vitabu vyao wao wenyewe ikiwemo vitabu vya Riwaya, Chombezo mbalimbali za Mapenzi Pamoja Vitabu vinavyohusu taaluma mbalimbali ikiwemo Uchumi, Jamii na Sheria, 

Kwa Bongo Writers kazi kwao ndio kwanza inaanza mategemeo yao makubwa ni kuwa na mawakala mikoa yote ya Tanzania, kwa sasa wakianzia Dar es salaam!! kwa sasa wanapatikana Ndani ya Ubungo bus terminal,

Mwandishi Daudi Mwidima (kulia) Mwandishi wa Riwaya ya "SIKU YA KWANZA KABURINI" akikabidhi nakala za kitabu chake kwa Wakala Suleiman kijogoo  (kushoto)

Kwa maitaji yako ya vitabu Jumla na rejareja, unaweza kutembelea banda lao ndani ya Ubungo Bus terminal, au unaweza kuwasiliana na wakala huyu kwa mawasiliano zaidi:

Kupitia namba hii 0678 683278

 



Comments

Popular posts from this blog

SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza

SIMULIZI : Aisha Toka Tanga sehemu ya Pili

JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?