Posts

The One Boy Group (Warembo na Watanashati

Image
Kutana na Kikundi cha One Boy Group (Warembo na Watanashati)  Na Daudi Mwidima:  Kikundi   hiki kinachoundwa na wasanii, wa maigizo,  Filamu pamoja na aina nyingine ya sanaa chenye maskani yake Mbagala Jijini Dar es salaam,  chenye Takribani Miezi Nane toka kuanzishwa kwake, kikiwa chini ya kiongozi wao "One boy" mwaka huu wa 2020 - 2021 kimejiwekea mikakati mbalimbali ya kisanii ikiwemo kuandaa Safari tour ya kuzunguka mikoa mbalimbali ya Nchini Tanzania lengo likiwa kutoa burudani na kuelimisha jamii kupitia kazi za sanaa wanazofanya, Pia kutoa video za maigizo pamoja na aina nyingine ya Filamu ambazo zitabeba maudhui ya uchekeshaji pamoja na kuelimisha jamii,  kupitia You tube channel na mitandao mingine ya kijamii.  Watanzania na nchi jirani sasa wakae mkao wa kula kupokea kazi za wasanii hawa ambao wamepania kuitikisa vilivyo sanaa ya bongo,  baada ya kufanya nao mahojiano nikiwa pamoja na Mkurugenzi wa kundi Mr.  One Boy na Msanii ...

SIMULIZI: THE JOKER - Muuaji wa Siri Sehemu ya kwanza hii Hapa

Image
 - THE JOKER (Muuaji wa Siri)  Sehemu ya Kwanza hii hapa: Katika Nchi ya Tanzania,  jijini Mwanza,  yapata saa tano za usiku, katikati mwa jiji la Mwanza eneo la Capri point,  mtaa wa sita kutoka barabara Kuu ya kuingia katika jengo la Benki Kuu ya Tanzania,  nyumba namba 43 nyumba ambayo geti lake lilikua la chuma kilichochakaa,  Upande wa ndani kulikua na nyasi nyingi zilizoonyesha hazijapata kufyekwa takribani miaka miwili, pembeni mwa jengo lile kulikua na gari bovu aina ya land Cruiser rangi ya bluu,   Lango la kuingilia ndani pembezoni kabisa mwa ukuta palikua na Pipa, ambalo ndani yake kulikua na karatasi zinaendelea kuwaka,  humo  ndimo alimojificha Joka Mtu,  au kwa jina lingine unaweza kumuita The Joker,  akiwa kasimama katika kioo kilichopasuka,  shingoni akiwa kajifunga mnyororo mrefu uliofika hadi kwenye kiuno kisha kurudi tena shingoni na kushuka hadi chini,  hakika ulionekana mnyororo mzito kwelikw...

SIMULIZI YA SIKU YA KWANZA KABURINI hii hapa

Image
Habari!? Kwa jina naitwa John Sindano, Mzaliwa wa Mkoa wa Mwanza, kijiji cha Buhima kata ya Ukiriguru, kaskazini mwa nchi ya Tanzania pembezoni mwa ziwa maarufu barani afrika, ziwa lenye samaki watamu aina ya Sato na sangara, likifahamika kama ziwa Nyanza, kwa wakazi wa Mwanza na sehemu nyingine jirani ya Tanzania, lakini kidunia likijulikana kama ziwa Victoria, hii ni baada ya malkia wa uingereza Queen Victoria kutembelea eneo hilo la ziwa yapata miaka elfu moja mia nane na hamsini nane (1858) iliyopita, Nadhani wengi wenu mlishawahi kusikia simulizi ya ziwa hili Kama sio kuisoma katika historia, moja ya maajabu ya ziwa hili ni kwamba, ndio ziwa pekee linalopokea maji yake toka mto Nile, nchini Libya na maji hayo hutiririka miaka nenda rudi toka Libya hadi katika ziwa Victoria, Sikuja hapa kukuelezea kuhusu historia ya nchi yetu ya Tanzania, Bali Nimejikuta naeleza yote hayo, baada ya wewe ndugu yangu kunionyesha Ukarimu wa Hali ya juu, Ukarimu ambao unapatikana nc...

BONGO WRITERS (UMOJA WA WAANDISHI WA VITABU) Vitabu ndio Mlezi wa Maendeleo

Image
  Dunia ikiwa inakimbizana na Maendeleo ya Sayansi na Tekinolojia, Haiwezi kuendelea mbele bila watu Kusoma vitabu na kupata maarifa ya kuweza kuwasaidia waweze kugundua vitu mbalimbali, na kufikia malengo makubwa ya kitekinolojia na kisayansi, Usomaji wa vitabu ndio sehemu Pekee ya binadamu kupanua mawazo yake na kufikia malengo anayayoyataka kimaendeleo iwe kiuchumi, kijamii hata kisiasa, Vitabu ni Mlezi wa maendeleo katika Nchi yoyote ile, tunaweza kusema Vitabu ndio "Mama wa maendeleo" kwani maarifa yote tunayotumia ili kuweza kupiga hatua za kimaendeleo, yamefichwa katika vitabu, Kuliona hilo Bongo Writer wamekuja na hili kusaidia na kuhamasisha usomaji wa vitabu Tanzania , Bongo Writers (BW) ni nini?   Bongo Writers ni Umoja wa waandishi wa Vitabu walioamua kuungana na kusimamia kazi zao kwa pamoja ikiwemo Kuuza vitabu vyao wao wenyewe ikiwemo vitabu vya Riwaya, Chombezo mbalimbali za Mapenzi Pamoja Vitabu vinavyohusu taaluma mbalimbali ikiwemo Uchumi, Jamii...

RIWAYA (NOVEL) SIKU YA KWANZA KABURINI SASA IPO MADUKANI

Image
Riwaya ya Simulizi ya Kugofya na kusisimua mwili "SIKU YA KWANZA KABURINI" sasa Imetoka na inapatikana Maduka yote ya Vitabu kwa Mawasiliano wasiliana na Mwandishi Daudi Mwidima kwa namba hizi kupata Nakala yako - 0656 337439 au 0754 542642 

Leo Katika Burudani - Vitali Maembe

Image
Leo Katika Burudani, tunae Vitali Maembe, msanii kijana toka Bagamoyo, maarufu kwa wimbo wa  "Sumu ya teja" wengi ukitaja wimbo huo wanaweza kua wanajua wimbo huo, bila kumjua msanii mwenyewe, hii inatokana na msanii huyu kupendelea zaidi kuimba nyimbo za jukwaani, ijapokua ana video kadhaa kama wimbo wa Katiba ambao ameshautolea video. Aina ya nyimbo zake ni kuhamasisha watu, kuipenda nchi yao ya Tanzania, kujitambua, kuhimiza utawala bora na mambo mengine yanayohusu maadili ya Mtanzania, baadhi ya nyimbo alizokwisha toa ni KUDU, VUMA, pamoja na KATIBA. Uwezo wake katika kupiga Gitaa akiwa anaimba ndio uliompa zaidi umaarufu, inasikitisha kwa upande mwingine wasanii wazuri kama Hawa kutowasikia tena na tukiacha wakipotea na nyimbo zao zenye mvuto katika kusikiliza na kujifunza. Nikipata kibali toka kwake nitaweka baadhi ya nyimbo zake hapa ili wengi wetu tupate kumjua zaidi. Makala hii imeandaliwa na Daudi Mwidima

VIDEO : Tujikumbushe Kutoka Bunge Lililopita