Posts

Showing posts from 2017

Leo Katika Burudani - Vitali Maembe

Image
Leo Katika Burudani, tunae Vitali Maembe, msanii kijana toka Bagamoyo, maarufu kwa wimbo wa  "Sumu ya teja" wengi ukitaja wimbo huo wanaweza kua wanajua wimbo huo, bila kumjua msanii mwenyewe, hii inatokana na msanii huyu kupendelea zaidi kuimba nyimbo za jukwaani, ijapokua ana video kadhaa kama wimbo wa Katiba ambao ameshautolea video. Aina ya nyimbo zake ni kuhamasisha watu, kuipenda nchi yao ya Tanzania, kujitambua, kuhimiza utawala bora na mambo mengine yanayohusu maadili ya Mtanzania, baadhi ya nyimbo alizokwisha toa ni KUDU, VUMA, pamoja na KATIBA. Uwezo wake katika kupiga Gitaa akiwa anaimba ndio uliompa zaidi umaarufu, inasikitisha kwa upande mwingine wasanii wazuri kama Hawa kutowasikia tena na tukiacha wakipotea na nyimbo zao zenye mvuto katika kusikiliza na kujifunza. Nikipata kibali toka kwake nitaweka baadhi ya nyimbo zake hapa ili wengi wetu tupate kumjua zaidi. Makala hii imeandaliwa na Daudi Mwidima

VIDEO : Tujikumbushe Kutoka Bunge Lililopita

SIMULIZI : Aisha Toka Tanga sehemu ya Pili

Image
Juma lililopita tuliona, Aisha akiwa amepata hifadhi katika bweni la wanafunzi la wavulana alipoingia chumbani na alipopanda tu kitandani akajikuta usingizi umempitia sasa endelea.............. Nikiwa nimesimama nje nikijiuliza jinsi nilivyofanya maamuzi ya gafla! Bila kufikiria, mara nilishtushwa na sauti ya mlinzi "Hussein!!!" nikageuka na kuangalia nyuma yangu, aha Mzee nilimuita, huyu mzee nilimfahamu nilipofika tu chuoni, tulitokea kijiji kimoja, na alinipokea na kunisaidia kujua mazingira ya chuo kabla hata sijapata marafiki,  ambao ni wanavyuo wenzangu, nilimuita Mzee sababu alipendwa kuitwa ivyo ingawaje umri wake haukua mkubwa sana alionekana ana umri Kati ya miaka 40 au 45 hivi. Mbona umesimama mwenyewe hapa", aliniuliza, nilibaki kumshangaa sababu sikujua kama ataniuliza swali hilo, mara nyingi alizoea utani, pia nilishtushwa kumuona, sikupenda ajue kama ndani kwangu Kuna mgeni tena mgeni ambae ni wa kike,  sababu hajawahi kuniona nikiwa nimesimama na wa...

Viongozi Kadhaa wa Chadema

Image
Kutoka kushoto ni Mh. Lomu, Msigwa, Mke wa Lissu, Mbowe, Kubenea, Mh Lema na mwenye suruali nyekundu ni dereva wa Tundu Lissu wakiwa katika picha ya pamoja Jijini Nairobi.

Mc Pilipili Apata Ajali Shinyanga

Image
Mchekeshaji na mtumbuizaji katika sherehe,  Immanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili, siku ya jana akiwa anaendesha gari aina ya Land Cruser rangi ya Silver, amepata ajali kijiji cha Bubiki/kata ya Mondo mkoa wa shinyanga baada ya kujaribu kumkwepa mtoto aliekua akikatiza barabarani na baiskeli, na kukimbizwa hospitali Bugando Jijini Mwanza. Afisa uhusiano wa hospitali ya Bugando Lucy Joseph amekiri kumpokea Mc Pilipili na anashughulikiwa katika kitengo cha dharula hospitalini hapo. Mc Pilipili alikua akitokea Jijini Mwanza kurudi Dar es salaam, kusherehesha sherehe, kamanda mkuu wa mkoa Shinyanga Simon Haule amekiri kutokea kwa ajali hiyo.

SIMULIZI : AISHA TOKA TANGA Sehemu ya kwanza

Image
Nakumbuka ilikua ni siku ya jumamosi nikiwa nimemaliza kufanya mazoezi ya kukimbia, katika kiwanja cha chuo kikuu Jijini Dar es salaam, kwa Kawaida huwa napenda sana kufanya mazoezi siku ya jumamosi, nizunguke Uwanja mara kumi na tano hadi ishirini, Kisha baada ya hapo narudi bwenini kwa ajili ya kuoga na kujiandaa kwenda katika madarasa kwa ajili ya kujisomea. Nikiwa mwanafunzi wa Ualimu katika kitivo cha Elimu,  mwaka wa pili,  chuoni hapo, na toka nifike chuoni sikupenda kua na marafiki, ivyo nilikua naishi maisha ya kujitenga na wanafunzi wenzangu muda wote, rafiki yangu mkubwa ilikua ni Elimu na mazoezi na kila nilikua nikifikiria hali ya kimaisha nyumbani jinsi ilivyo duni, niliona ni bora nisome kwa bidii ili nije kuwasaidia nyumbani. Sikupenda kabisa kua na marafiki, maana niliogopa wanaweza kunivurugia ndoto zangu za kufikia malengo yangu. Nikiwa bado na hema kwa nguvu kutokana na kumaliza kukimbia gafla!! Mvua ilianza kunyesha nikiwa nipo kifua wazi nimevaa bukta...

Rais Magufuli - SITATOA HUKUMU YA KIFO KWA WAFUNGWA

Image
Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli, katika hotuba yake ya kumuapisha Jaji mkuu Mpya wa Mahakama za Tanzania, Prof Ibrahim Khamis Juma, sherehe iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Rais Magufuli, alisisitiza kua hatoweza kusaini orodha hiyo ya kifo kwa wafungwa walio hukumiwa kunyongwa, alisema "nafahamu wapo wafungwa wengi huko magerezani, sisi wanasiasa tu naogopa sana kutoa hukumu hii ya kunyonga" Pia katika hotuba yake alisema kuchelewa kumteua Jaji mkuu wa Mahakama, ni kuhakikisha anateua mtu makini atakaeweza kupambana na Rushwa katika kasi anayoitaka. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Khamis Juma amekua Jaji wa 7 toka Tanzania ipate uhuru mwaka 1961

NDOTO MBAYA - NIGHTMARE sehemu ya 2

Image
Katika makala yaliyopita, tuliona jinsi ambavyo mtu anaweza kujikuta anaota ndoto mbaya, (bad dream) au nightmare, kutokana na mazingira ya chumba alicholala, niligusia vitu baadhi ikiwemo chumba kutokua kisafi, kujaza vitu vingi chumbani nk, sasa endelea........ Sababu ya tatu ya mtu kujikuta anaota ndoto mbaya, inaweza kusababishwa na matukio ya kimaisha, ya kila siku hapa nitagawa matukio ya kimaisha katika pande kuu mbili (2) : (1) Aina ya Kazi (2)Aina ya mazingira Aina ya kazi - hii inaweza kua chanzo cha mtu kuota ndoto mbaya pindi aingiapo kulala, mfano, mtu anafanya kazi ya mochwari mara nyingi anajikuta anahusika na kutunza miili ya marehemu, hii hupelekea mtu huyo kuota ndoto mbaya,  anaweza kujikuta anaota,  aidha amekaa na marehemu nk. Hali hii pia huwatokea watu wanaofanya kazi katika maeneo hatarishi, kama katika majengo marefu, anaweza kuota anadondoka nk, au mitambo mikubwa ya viwandani nk. Tukumbuke ubongo wa Binadamu una tabia ya kupokea kila kitu u...

KAMPUNI YA YONO YAUZA JUMBA LA LUGUMI

Image
Jumba la kifahari lililokua linamilikiwa na Lugumi enterprises, limepigwa mnada na kampuni ya Yono enterprises, jumba hilo linalopatikana Upanga Jijini Dar es salaam limenunuliwa na kampuni ya Al-Naeen enterprise kwa thamani ya Tshiling milioni 700. Jumba hilo ni sehemu ya nyumba nyingine mbili za Lugumi , zinazopigwa mnada zinazopatikana Mbweni JKT wilaya ya KINONDONI,  Jijini Dar es salaam ambazo bado hazijapata wanunuzi hadi sasa ambazo thamani yake ni Tshiling milioni 460 kwa kila nyumba moja,  bei ambayo imeelezwa ni kubwa tofauti kabisa na ukubwa wa nyumba hizo. Uamuzi huo umekuja baada ya kampuni ya Lugumi enterprises kushindwa kulipa kodi na ubadhilifu mwingi uliofanywa na Lugumi, sehemu ya fedha hizo zitatumika kulipia kodi TRA.

Mh. KASSIM MAJALIWA - Thamani ya Dhahabu Nyeupe irudi

Image
Waziri mkuu wa Tanzania, mh. Kassim Majaliwa akiwa mjini Dodoma alifanya mkutano na wakuu wa mikoa inayoongoza kuzalisha zao la Pamba, ikiwemo mkoa wa Mara, Mwanza, Simiyu, Morogoro, Shinyanga pamoja na singida. Katika mkutano huo waziri Mkuu kassim Majaliwa, aliwataka wa kuu wa mikoa hiyo kua na Agenda moja ya kuinua kwa pamoja zao la Pamba ambalo lilijulikana kama "Dhahabu Nyeupe",  sifa ambayo ilipotea baada ya changamoto ya nguo kutoka nchi za nje, pamoja na Mabadiliko ya Hali hewa pamoja na kitekinolojia. Kama ambavyo serikali ya Awamu ya tano ya Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli, ikisisitiza kuhusu "uchumi wa viwanda", jitahada izo za kuinua uchumi zinaenda pamoja na kuinua kilimo haswa zao la biashara ambalo tayari lilikua limeanza kupotea. Waziri mkuu pia alisisitiza kuhusu utaratibu wa kuinua zao hilo, lazima uanzie katika utaratibu wa kuchagua mbegu bora, matayarisho ya shamba hadi kufikia hatua ya kuvunwa na kuuzwa. "lazima kila mkoa uwe na af...

KIBWAGIZO

Image

JE? UNAJUA POMBE ZA BEI GHARI DUNIANI?

Image
Hili linaweza kuonekena kama kichekesho au mshangao,  kwa watu wengine haswa kwa wale  ambao kipato Chao ni cha kawaida au cha Kati, ila kwa matajiri wapenda starehe jambo hili Kwao ni la kawaida kabisa, waswahili wanasema,  "ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauni"  sasa ungana na mimi kujua baadhi ya Pombe nikimaanisha aina yoyote ya kilevi iwe wine, wisky, grants, beer n.k zenye bei kubwa Duniani. Hii ni Richebourg Grand Chuck, iliyotengenezwa na Henry Jayer miaka ya 1978, bei yake kwa thamani ya kitanzania ni Milioni 47!!!! Hahaha najua unashangaa maana milioni 47 kwa Tanzania inatosha kabisa kujenga nyumba ya kawaida na kununua gari ndogo ya kutembelea. Tukiachana na Richebourg Grand Chuck ambayo ndugu msomaji,  unaweza kubisha kua haiuzwi bei hiyo, basi ngoja nikuletee aina nyingine ya Pombe hii imeandikwa hadi lebo ya bei kwa thamani ya pesa za kitanzania nayo ni hii hapa: Hennessy,  ikiwa na Lebo iliyoandikwa Milioni 2 na laki 5 za kit...

MAANA YA NDOTO MBAYA : NIGHTMARE

Image
Nadhani wengi wenu mmewahi kusikia kuhusu Ndoto mbaya au Ndoto za kutisha, leo katika blog hii, tuta angalia kwa kina nini hasa usababisha ndoto mbaya au kama inavyojulikana kwa lugha ya kiingereza "nightmare" Ndoto Mbaya ni nini? - hili ni swali linaloweza kujibiwa na mtu yoyote aliyepitia ama kuota ndoto mbaya, wapo watu wanafananisha ndoto mbaya na Nguvu za giza, yaani uchawi, wapo wengine wana amini ndoto mbaya zinatokana na ishara toka kwa mungu, hawa ni wale wanao amini kwa mungu, wapo wanao amini ndoto mbaya zinatokana na mizimu (marehemu), pia wapo wanaosema ndoto mbaya zinatokana na matendo ya mtu mwenyewe yaani kama mtu anafanya matendo mabaya, basi pia mtu huyo lazima ataota ndoto mbaya. Hizo ni imani mbali mbali za watu tofauti kutokana na utafsiri wao katika ndoto, siwezi kusema wapo sahihi au hapana ila kwa sasa tuangalie kitu gani kinachosababisha ndoto mbaya/ nightmare. Chanzo cha ndoto mbaya: Tafiti mbali mbali, kuhusu mwili wa Binadamu zinaonyesha k...

VIDEO : Mazungumzo ya Makinikia yakiendelelea Jijini Dar es salaam

BURUDANI : JE? UNAMJUA DJ KHALED Hii ni historia yake fupi

Image
DJ Khaled, wengi humtambua kwa jina hilo ila jina lake halisi ni "Khaled Mohammed  Khaled" alizaliwa November 26, 1975 bila shaka umri wake utakua miaka 42 hivi sasa, kabla ya kuitwa DJ Khaled alijulikana kwa majina tofauti tofauti kama vile, "Beat Novacana, na Arab Attack, jina la Arab attack aliamua kulibadilisha baada ya kutokea kwa shambulio la kigaidi la tarehe 9/11/2001,  nchini marekani. DJ Khaled alianza shughuli za Muziki akiwa kama" DJ" na ndio sababu ya jina lake kuanzia na neno DJ, kazi ambayo kwa mujibu wa jarida la foxy,  alikiri kua anaipenda kazi hiyo hadi sasa, pia ni Rapper, song writer na sasa ni Producer, uwezo wake pia katika kucheza vifaa vya Muziki haupo nyuma anaweza kucheza vifaa mbali mbali ikiwemo kinanda, na guitar. Tangu aanze Muziki alishapitia kampuni mbali mbali za kimuziki ikiwemo Young money, Cash money, pamoja na Def Jam south, lakini kwa sasa ana kampuni yake mwenyewe inayojulikana kwa title kubwa ya "Another On...

MCHUNGAJI GWAJIMA KUMUOMBEA TUNDU LISSU

Image
Siku ya Jana tarehe 8/09/2017,  mchungaji Joseph Gwajima,  alitangaza kufanya maombi maalum,  kumuombea mwanasheria mkuu wa Chadema ambae,  pia ni Rais wa Tanganyika law society (TLS) Tundu Antipas Lissu, aliyejeruhiwa kwa kupigwa Risasi mjini Dodoma siku ya tarehe 7/09/2017 Alhamisi na watu wasiojulikana na kukimbizwa hospitali ya Dodoma na baadae kusafirishwa na ndege ya Dharula kwenda nchini Kenya, Nairobi katika hospitali ya Aga - khan kwa matibabu zaidi, maombi hayo yatafanyika  kanisani kwake,  Ubungo maarufu kama kanisa la ufufuo na uzima. Mchungaji Joseph Gwajima ni mmoja ya wachungaji nchini Tanzania anaefuatilia kwa umakini mkubwa Hali ya kisiasa Tanzania na kukemea na kuonya pale inapobidi Hali inayopelekea kugongana na vyombo vya dola mara kwa mara.